Machapisho

Picha
TADB KUWASHIKA MKONO WAHITIMU VYUO VIKUU. Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB)imeazimia kuwashika mkono wahitimu wa vyuo vikuu hususani waliosomea masomo yanayohusu kilimo na uvuvi kwa kuwapatia mikopo mbalimbali ili waweze kutekeleza kwa vitendo vile walivyojifunza machuoni. kwa kufanya hivyo wanaamini watachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana sambamba na kukuza uchumi wa viwanda kupitia hiyo miradi itakayofanywa na hao wahitimu kwa kupitia hiyo mikopo itakayotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo.  Hivyo, sisi blog ya "ngalibanews" tunaipongeza benki ya maendeleo ya kilimo kwa kuwapatia hiyo fursa vijana ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kuthubutu na kuchangamkia hiyo fursa. Pia tunawashauri hao wahitimu katika masomo ya kilimo na uvuvi kujiunga pamoja na kuunda kikundi chao ambacho watakisajili kwa mujibu wa sheria na muongozo wa idara ya maendeleo ya jamii ili iwe rahisi kwao kupata huo mkopo na kutekeleza miradi yao a...
Picha
 TENGERU MARKET SACCOS KAA LA MOTO LA MAENDELEO Vyama vya Ushirika bado vina nafasi muhimu katika kuwaunganisha na kuwawezesha wananchi kubadili maisha yao na kujiendeleza kiuchumi.Aidha, Vyama vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) ni nyenzo ya kuwapatia wananchi mitaji kutokana na michango yao na mikopo kutoka katika vyombo na taasisi za fedha. TENGERU MARKET SACCOS NI NANI? Hiki ni chama cha ushirika kilichoundwa kwa umoja wa wafanyabiashara wanaopatikana katika soko la Tengeru lililopo wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha. Lengo la chama hiki cha ushirika nikubadili maisha ya wafanyabiashara hao kwa kuwaendeleza kiuchumi kwa kuwapatia mikopo mbalimbali itokanayo na michango yao kwa ajili ya kukuza biashara zao. KWANINI NI KAA LA MOTO? Tengeru market saccos ni kaa la moto la maendeleo kwa wanachama wake kwa sababu wameshindwa kutimiza lengo walilolikusudia pindi kinaanzishwa hiki chama.kwa takribani miaka zaidi ya mitano saccos hii ya soko la Tengeru haitoi huduma...
Picha
KILICHOPO NYUMA YA PESA ZA VIJANA NA WANAWAKE HALMASHAURI  Kwenye kila halmashauri nchini Tanzania kuna pesa zimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake. Pesa hizo zimetengwa kwa ajili ya kuwapa vikundi vya kimaendeleo ambavyo vimeundwa na hao vijana pamoja na hao wanawake. Na ili kila kikundi kiweze kupata hizo pesa ni lazima kiwe na shughuli maalumu ya uzalishaji mali ambazo zinawaingiza kipato sambamba na hivyo vikundi kutambulika kisheria yaani visajiliwe katika ofisi zenye mamlaka husika ambazo zipo chini ya usimamizi wa afisa maendeleo.   KWANINI VIJANA NA WANAWAKE? Kwa sababu haya makundi mawili ndio chachu ya maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla kwa kuwa vijana ni taifa la kesho hivyo hakuna budi kuwawezesha sasa ili kesho waweze kusimama wenyewe na ukimuwezesha mwanamke mmoja ni sawa umeiwezesha jamii nzima kwa kuwa wanawake wanaangaliwa kama chachu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla kulingana na walivyobarikiwa. ...
Picha
    DHANA YA VIKUNDI VYA MAENDELEO NA ASASI ZA KIBENKI Katika jamii kuna vikundi vya maendeleo na vikundi hivi vya maendeleo kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa vinatengeneza fursa mbalimbali kwa wanachama na jamii kwa ujumla kupitia huduma au bidhaa zao. MAANA YA VIKUNDI VYA MAENDELEO Vikundi vya maendeleo ni vikundi vyote vinavyojihusisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika jamii yaani vikundi hivi vinakuwa na kazi zao maalumu wanazozifanya ambazo zinawaingiza kipato na kuwasaidia katika jitihada zao za kupambana na umaskini.mfano wa shughuli zinazofanywa na hivi vikundi vya maendeleo ni ukulima wa mazao,ufundi seremala na ufundi washi,utengenezaji wa sabuni na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu na shughuli nyingine nyingi sana. IDADI YA WATU Kumbuka hivi ni vikundi kwa ajili ya kutengeneza faida ili wanachama wake waweze kujikwamua na changamoto mbalimbali katika maisha yao sambamba na umaskini.hivyo wataalamu wa maendeleo ya jami...
Picha
HUYU NDIO MZAZI WA VICOBA(VILLAGE COMMUNITY BANK) VICOBA NI NINI??  Vicoba(village community bank) ni benki za kijiji zilizoanzishwa na watu kuanzia 15 mpaka 30 kwa lengo la kuweka akiba na kukopeshana kwa riba nafuu ambayo watakuwa wamekubaliana wanachama wenyewe kwa mujibu wa katiba yao. lengo la kuanzisha hizi benki ni kusaidiana ili waweze kupambana na umaskini sambamba na changamoto mbalimbali za kimaisha hasa za kiuchumi na kijamii.  vicoba uendeshwa kwa katiba maalumu kulingana na makubaliano ya wanachama na pia katiba hizo lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria na kanuni za wizara husika kuanzia ngazi ya kata mpaka wilaya. MZAZI WA VICOBA  "UPATU" ndio mzazi wa VICOBA(village community bank). Upatu ni mchezo unaotumiwa na watu mbalimbali kuchangiana fedha kisha baada ya fulani hizo fedha anapewa mtu na kuanza kuchangiana tena kwa ajili ya kupewa mtu mwingine kwa maana hizo fedha zinazochangishwa utolewa kwa mzunguko ili kilaaliyechangia lazima apate. le...
Picha
RC KILIMANJARO AWAAMSHA WALIOLALA MKOANI HUMO. MOSHI, KILIMANJARO Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro mheshimiwa Mama Anna Mgwira amewaamsha wanawake wa mkoa huo kuchangamkia fursa zinazopatikana katika taasisi za kifedha zinazotoa huduma za kibenki ili waweze kupata huduma hizo hususani za kupata mkopo nafuu utakaowawezesha kujikita katika shughuli za kiujasiliamali ili waweze kujiingizia kipato. Mkuu wa mkoa huyo aliyasema maneno hayo wakati alipokuwa akizindua jukwaa la wanawake katika mkoa huo. Alisema kuwa "kuna biashara nyingi tunazoweza kufanya hususani ya kusindika matunda maana biashara hiyo imekuwa ikishika hatamu duniani kote, hivyo tutumie hizo taasisi za kifedha zinazotoa huduma za kibenki ili tuweze kufanya hiyo biashara". Hivyo sasa ni wakati pia kwa taasisi hizo za fedha zinazotoa huduma za kibenki kuwafuata wananchi na kuzungumza nao kwa kina uku wakiwapa uelewa wa kutosha juu ya mchango wa hizo taasisi zao katika maisha ya mwananchi ili waweze kuzitumia ...
Picha
   opportunity for higher learning students and secondary students in Tanzania. Dar es salaam, Tanzania. The Dar es salaam Stock Exchange(DSE) introducing Scholar Investment Challenge for targeting Tanzanian youth in higher learning institutions. The challenge is an online simulation of live trading at the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE), where each participating group or individual is given a virtual start-up capital to invest using the DSE real time information for a period of 3 months.  The winner is the team or individual considered by a panel of judges to have made the most sound investment decisions, the highest portfolio value and to have contributed in the discussion forum. The DSE scholar investment Challenge 2017 is open to any Tanzanian youth who is enrolled in any higher leaning Institution in the country. The main objectives of the challenge are to develop and encourage the culture of saving and investment as well as to enhance financial ...