Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB)imeazimia kuwashika mkono wahitimu wa vyuo vikuu hususani waliosomea masomo yanayohusu kilimo na uvuvi kwa kuwapatia mikopo mbalimbali ili waweze kutekeleza kwa vitendo vile walivyojifunza machuoni. kwa kufanya hivyo wanaamini watachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana sambamba na kukuza uchumi wa viwanda kupitia hiyo miradi itakayofanywa na hao wahitimu kwa kupitia hiyo mikopo itakayotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo.
Hivyo, sisi blog ya "ngalibanews" tunaipongeza benki ya maendeleo ya kilimo kwa kuwapatia hiyo fursa vijana ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kuthubutu na kuchangamkia hiyo fursa. Pia tunawashauri hao wahitimu katika masomo ya kilimo na uvuvi kujiunga pamoja na kuunda kikundi chao ambacho watakisajili kwa mujibu wa sheria na muongozo wa idara ya maendeleo ya jamii ili iwe rahisi kwao kupata huo mkopo na kutekeleza miradi yao ambayo itachochea maendeleo ya nchi yetu kuelekea uchumi wa kati na uchumi wa viwanda.
Maoni
Chapisha Maoni