TENGERU MARKET SACCOS KAA LA MOTO LA MAENDELEO
Vyama vya Ushirika bado vina nafasi muhimu katika kuwaunganisha na kuwawezesha wananchi kubadili maisha yao na kujiendeleza kiuchumi.Aidha, Vyama vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) ni nyenzo ya kuwapatia wananchi mitaji kutokana na michango yao na mikopo kutoka katika vyombo na taasisi za fedha.
TENGERU MARKET SACCOS NI NANI?
Hiki ni chama cha ushirika kilichoundwa kwa umoja wa wafanyabiashara wanaopatikana katika soko la Tengeru lililopo wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha. Lengo la chama hiki cha ushirika nikubadili maisha ya wafanyabiashara hao kwa kuwaendeleza kiuchumi kwa kuwapatia mikopo mbalimbali itokanayo na michango yao kwa ajili ya kukuza biashara zao.
KWANINI NI KAA LA MOTO?
Tengeru market saccos ni kaa la moto la maendeleo kwa wanachama wake kwa sababu wameshindwa kutimiza lengo walilolikusudia pindi kinaanzishwa hiki chama.kwa takribani miaka zaidi ya mitano saccos hii ya soko la Tengeru haitoi huduma kwa wanachama wake na kibaya zaidi viongozi wa saccos hii imefunga ofisi ikiwa na pesa nyingi za wanachama wake zilizotokana na michango yao kwa kununua hisa na kuweka akiba. Blogu hii ilifanya mahojiano na baadhi ya wanachama wa saccos hii na kuthibitisha ukweli wa hizo tuhuma na kwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa viongozi wa hiyo saccos ndio wanamaisha mazuri kwa maana wanamiliki miradi mingi ya ufugaji,mali zisizo hamishika kama nyumba na viwanja. kwa hali ilivyo ina sadifu fika kuwa saccos hii ya Tengeru market ni kaa la moto la maendeleo kuelekea uchumi wa viwanda na inakwamisha kwa kiwango kikubwa jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha maisha ya watu wake kupitia kuanzishwa vyama vya ushirika.
NINI KIFANYIKE?
Ikumbukwe kuwa vyama vingi vya ushirika vinahifadhi pesa zao katika ofisi zao hali inayopelekea kuwepo kwa ubadhilifu wa mali za wanachama. Hivyo, asasi za fedha zinazotoa huduma za kibenki hazina budi kushirikiana kwa karibu na hivyi vyama vya ushirika katika kuhakikisha wanakomesha hizi changamoto zinazozikabili hivi vyama vya ushirika kwa maana utoaji wa fedha katika asasi za fedha zinazotoa huduma za kibenki zina utaratibu maalumu wa kutoa pesa kulingana na utaratibu wa katiba ya chama na pia unatunza kumbukumbu ambazo zinakuja kuwa msaada pindi wa ukaguzi wa taarifa za fedha na mali za chama. Pia elimu ya utawala bora itabidi itolewe ili kuleta uweledi na ufanisi wa kazi kwa viongozi wa vyama husika kwa kujua kuwa wanafanya kazi kwa ajili ya watu na si wao binafsi. kwa kufanya hivo kutasaidia sana nchi yetu kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Maoni
Chapisha Maoni