KILICHOPO NYUMA YA PESA ZA VIJANA NA WANAWAKE HALMASHAURI
 Kwenye kila halmashauri nchini Tanzania kuna pesa zimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake. Pesa hizo zimetengwa kwa ajili ya kuwapa vikundi vya kimaendeleo ambavyo vimeundwa na hao vijana pamoja na hao wanawake. Na ili kila kikundi kiweze kupata hizo pesa ni lazima kiwe na shughuli maalumu ya uzalishaji mali ambazo zinawaingiza kipato sambamba na hivyo vikundi kutambulika kisheria yaani visajiliwe katika ofisi zenye mamlaka husika ambazo zipo chini ya usimamizi wa afisa maendeleo.
 
KWANINI VIJANA NA WANAWAKE?
Kwa sababu haya makundi mawili ndio chachu ya maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla kwa kuwa vijana ni taifa la kesho hivyo hakuna budi kuwawezesha sasa ili kesho waweze kusimama wenyewe na ukimuwezesha mwanamke mmoja ni sawa umeiwezesha jamii nzima kwa kuwa wanawake wanaangaliwa kama chachu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla kulingana na walivyobarikiwa.
 
KIPI KIPO NYUMA YA PESA ZAO?
Pesa hizo ni asilimia tano (5%) kwa wanawake na asilimia tano (5%) kwa vijana. Lakini cha kushangaza hao wanawake na vijana hawajui kwa namna gani waweze kunufaika na hizo pesa zao ambazo wametengewa kwa lengo kujiletea maendeleo yao wao wenyewe. Hivyo, kilichopo nyuma ya hizo pesa za vijana na wanawake ni vipaumbele vya serikali ya nchi ambavyo wameviweka kwa lengo la kuliletea taifa maendeleo. Kwa maana hiyo kushindwa kwa vijana na wanawake kutambua na kuelewa kwa kina vipaumbele vya serikali vimepelekea ugumu kwa namna moja ama nyingine kwa vijana na wanawake kunufaika na hizo pesa.
 
UTAJUAJE VIPAUMBELE VYA SERIKALI?
Kujua vipaumbele vya serikali ni lazima uwe Dira ya maendeleo ya taifa (2025) na Ilani ya chama cha mapinduzi (C.C.M) ambayo kwa uwazi kabisa vimejieleza na kufafanua kwa kina. Kwa maana hiyo miradi mbalimbali inayotekelezwa katika taifa letu inazingatia na kutekeleza dira ya taifa ya maendeleo na ilani ya chama cha mapinduzi (C.C.M).
 
NINI KIFANYIKE?
Vijana na Wanawake wanapaswa kuacha kufanya mambo kwa mazoea kwa sababu kunawafanya washindwe kuzitumia fursa zinazowazunguka ipasavyo. Hivyo, ata kuunda kwao vikundi ni lazima kuwe na tija ambayo itawawezesha kwa namna moja ama nyingine kupiga hatua kutoka sehemu ndogo kwenda sehemu kubwa kwa sababu kutawawezesha pia kunufaika na asasi mbalimbali za fedha zinazotoa huduma za kibenki kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.Hivyo, hatuna budi kubadilika na kufanya mambo yetu kwa ufasaha na uweledi zaidi kulingana na miongozo ya taifa letu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maana ya microfinance institutions(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki), imeandaliwa na Florian Lisso