RC KILIMANJARO AWAAMSHA WALIOLALA MKOANI HUMO.

MOSHI, KILIMANJARO

Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro mheshimiwa Mama Anna Mgwira amewaamsha wanawake wa mkoa huo kuchangamkia fursa zinazopatikana katika taasisi za kifedha zinazotoa huduma za kibenki ili waweze kupata huduma hizo hususani za kupata mkopo nafuu utakaowawezesha kujikita katika shughuli za kiujasiliamali ili waweze kujiingizia kipato. Mkuu wa mkoa huyo aliyasema maneno hayo wakati alipokuwa akizindua jukwaa la wanawake katika mkoa huo.

Alisema kuwa "kuna biashara nyingi tunazoweza kufanya hususani ya kusindika matunda maana biashara hiyo imekuwa ikishika hatamu duniani kote, hivyo tutumie hizo taasisi za kifedha zinazotoa huduma za kibenki ili tuweze kufanya hiyo biashara".

Hivyo sasa ni wakati pia kwa taasisi hizo za fedha zinazotoa huduma za kibenki kuwafuata wananchi na kuzungumza nao kwa kina uku wakiwapa uelewa wa kutosha juu ya mchango wa hizo taasisi zao katika maisha ya mwananchi ili waweze kuzitumia kwa mustakabali wa maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maana ya microfinance institutions(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki), imeandaliwa na Florian Lisso