DHANA YA VIKUNDI VYA MAENDELEO NA ASASI ZA KIBENKI
Katika jamii kuna vikundi vya maendeleo na vikundi hivi vya maendeleo kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa vinatengeneza fursa mbalimbali kwa wanachama na jamii kwa ujumla kupitia huduma au bidhaa zao.

MAANA YA VIKUNDI VYA MAENDELEO
Vikundi vya maendeleo ni vikundi vyote vinavyojihusisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika jamii yaani vikundi hivi vinakuwa na kazi zao maalumu wanazozifanya ambazo zinawaingiza kipato na kuwasaidia katika jitihada zao za kupambana na umaskini.mfano wa shughuli zinazofanywa na hivi vikundi vya maendeleo ni ukulima wa mazao,ufundi seremala na ufundi washi,utengenezaji wa sabuni na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu na shughuli nyingine nyingi sana.

IDADI YA WATU
Kumbuka hivi ni vikundi kwa ajili ya kutengeneza faida ili wanachama wake waweze kujikwamua na changamoto mbalimbali katika maisha yao sambamba na umaskini.hivyo wataalamu wa maendeleo ya jamii wanaopatikana katika halmashauri za nchi yetu wanashauri kwamba idadi nzuri ya wanachama kwa ajili ya vikundi vya maendeleo ni watu 10 mpaka 15 kwa sababu iwe rahisi kwa kila mmoja kunufaika na shughuli wanazozifanya za uzalishaji mali.

VIKUNDI VYA MAENDELEO NA HUDUMA ZA KIBENKI
Asasi nyingi za fedha zinazotoa huduma za kibenki wametupia macho yao katika hivi vikundi vya kimaendeleo kutokana na shughuli zao wanazofanya za uzalishaji mali. kwahiyo, hizo shughuli zinawapa fursa ya kupata huduma za kibenki kama vile mikopo, kuweka akiba,huduma za bima pamoja na kuhamisha pesa kama  kikundi au mtu mmoja mmoja. kwa kudhihirisha hilo katika halmashauri zetu nchini kote wanatoa mikopo ya gharama nafuu kupitia ofisi ya maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake watoto na wazee kwa sababu kuna pesa zimetengwa kwa ajili ya vikundi vya maendeleo.

MWISHO
Maendeleo katika jamii zetu tunajiletea wenyewe na sio kuletewa, kwa hiyo wakati umefika sasa kwa vijana,wanawake na wanaume kujiunga kwa pamoja na kuunda kikundi cha maendeleo kwa ajili ya uzalishaji mali na urahisi wa kupata huduma za kibenki kwa ajili ya kupambana na changamoto mbalimbali za kimaendeleo hususani umaskini.kwa hiyo, hizo asasi za fedha zinazotoa huduma za kibenki zimetoa kipaumbele kwa vikundi vya kimaendeleo kwa kufanya nao kazi ili waweze kuwanufaisha kwa namna moja ama nyingine na kuhakikisha kila siku jamii zetu zinakuwa na maendeleo.                                                                           

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maana ya microfinance institutions(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki), imeandaliwa na Florian Lisso