NAMNA YA KUNUFAIKA KUPITIA MICRO FINANCE INSTITUTIONS(TAASISI ZA FEDHA ZINAZOTOA HUDUMA ZA KIBENKI) 


Kuna manufaha mengi sana tunayoweza kupata pindi tu tutakapoamua kujikita sawa sawa katika kutumia hizi taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki. Na manufaha hayo tunaweza kuyapata kwa sababu idadi ya watu walio wengi wanaamini kuwa micro finance(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki) ni mkombozi wao kwa namna moja ama nyingine kuelekea kutimiza malengo yao na kuijenga kesho yao hapa chini ya jua.

Hivo manufaha mengi tunayoweza kuyapata kwa kiwango kikubwa yanachagizwa mno na huduma za kibenki zinazotolewa na taasisi hizo za fedha yaaani micro finance. Kwahiyo kupitia huduma za kibenki zifuatazo zinapelekea sisi watumiaji tunufaike au tupate manufaha.

1. Tunaweza kunufaika kwa kupata mkopo (loans access)

 
mara nyingi mkopo huu unakuwa rahisi kwa sababu ya kuwepo na kiwango kidogo cha riba ambacho kwa mtu yoyote atakapoenda kuomba na kupata anaweza akaurejesha. hivo kuna taratibu na kanuni pamoja na vigezo unapaswa kuvitimiza ili uweze kupatiwa huu mkopo. Manufaha ya huu mkopo ni kwamba unaweza kutusaidia kufanya mambo ya kimaendeleo hususani katika kuanzisha biashara yako mwenyewe itakayokuwezesha kujizalishia kipato maradufu.

2. Tunaweza kunufaika kwa kuweka akiba(savings)
kupitia hizi micro finance(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki) tunaweza kunufaika kwa kuweka akiba ya pesa zetu ili tuondokane na matumizi yasiyo na msingi na ulazima pia. kitendo cha kuweka akiba kinatupa nafasi ya kuja kutumia pesa zetu kwa wakati ujao tena kwa usahihi zaidi ili tuweze kufanyia jambo la msingi na lenye tija kwa faida ya maisha ya baadae.

3. Tunaweza kunufaika kwa kuhamisha pesa(money transfer)
kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani kumesaidia sana kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali ata ukiwa mahali ambapo ni mbali na ulipo. hivo kupitia micro finance kunatunufaisha kwa kuweza kuhamisha pesa kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine, nchi moja kwenda nyingine na ata bara moja kwenda bara jingine tena kwa uaminifu wa kiwango cha juu.

4. Tunaweza kunufaika kwa huduma za kibima(insurance services)
bima tunayoipata kupitia micro finance institutions(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki) ni bima ya mkopo na kuweka akiba katika taasisi yao na hiyo bima inatumika kukusaidia hasa pale utakapokopa pesa kisha ikatokea kwa bahati mbaya ukafariki duniani moja kwa moja akiba na bima yako ndo itaenda kuziba lile deni lililokuwepo pale ofisini kwao. pia kuna bima za aina nyingi ambazo unaweza kunufaika nazo pindi tu utakapojikita kutumia hizi taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki.

Kwahiyo haya ni machache kati ya mengi ambayo tunaweza kunufaika kwa namna mbalimbali kupitia kuzitumia hizi taasisi za kifedha zinazotoa huduma za kibenki yaaani micro finance.

pia tunaomba husisahau kumwalika na mwenzio aweze kupitia blog hii maridhawa ili aweze kujikusanyia madini mbalimbali yatakayomuwezesha kuibuka na kitu cha thamani sana.

napenda kuwatakia heri ya sikukuu ya pasaka na mapumziko mema......

















































































































































































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maana ya microfinance institutions(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki), imeandaliwa na Florian Lisso