waziri mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa

Waziri mkuu amwaga neema kwa taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki Tanzania.


MAGOGO, GEITA.

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ametoa baraka sambamba na kumwaga neema kwa taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki kutoa huduma hizo kwa wateja ambao ni wanunuzi wakuu wa zao la pamba mkoani geita na mikoa ya jirani.

Akisema maneno hayo katika sherehe za uzinduzi wa mbio za mwenge za uhuru mkoani humo, "mheshimiwa waziri mkuu alisema kuwa kwa sasa zao la pamba limekuwa jingi sana na sisi kama serikali kwa kushirikiana na wadau wetu tutahakikisha kuwa zao hili linanunuliwa lote kwa ajili ya maendeleo ya viwanda vyetu, hivyo taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki zitumie fursa hiyo kutoa huduma zao hususani za mikopo kwa watu".

Pia amehimiza wakulima kwa pamoja kujiunga na vyama vya ushirika ambavyo vitawasaidia katika kuendesha shughuli zao ili waweze kutimiza malengo yao kwa sababu kupitia hivo vyama vya ushirika wanaweza kunufaika kupitia huduma mbalimbali watakazozipata uko zikiwemo zile huduma za kibenki.

 Hivyo hii ni fursa kwa taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki kujipambanua zaidi kwa watu kupitia kutoa huduma zao ili kuendelea kukuza na kupanua soko lao.



husisahau kushare taarifa kwa watu wengine zaidi ili waweze pata madini ya kutosha.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maana ya microfinance institutions(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki), imeandaliwa na Florian Lisso