VIJUE VYANZO VYA MITAJI KWA AJILI YA MICRO FINANCE INSTITUTIONS.
Ikumbukwe kuwa kuna micro finance institutions( taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki) nyingi sana na miongoni mwa hizo taasisi za fedha ni saccos(saving and credits cooperatives), vicoba( village community bank),FINCA, pride na nyingine nyingi. Lengo kubwa la kuanzisha hizi taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki ni kufikia watu wote ambao hawana sifa za kupata huduma za kibenki katika mabenki ya kibiashara. Na hizi taasisi zinazotoa huduma za kibenki zikaenda mbali sana kwa kuboresha huduma zao ambazo zinampa mtu yoyote fursa ya kujiandalia kesho yake hususani katika kupambana kujikwamua na umaskini.
Sasa ili hizi taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki ziweze kujiendesha kwa kutoa huduma za kibenki kwa kila mtu lazima iwe na mtaji wa kutosha utakaowawezesha kujiendesha kwa uzuri ili mwisho wa siku iweze kuwa na tija kwa namna moja ama nyingine. Vifuatavyo ni vyanzo ambavyo hizi micro finance(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki) huwa wanavitumia ili kupata mitaji ya kuendesha shughuli zake.
mikopo ya mabenki(banks loans); mara nyingi mabenki ya kibiashara(commercial banks) ndo huwa wanawapa hiyo mikopo hizo taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki kwa kiwango flani cha riba ambacho kinakuwa kimepangwa kutokana na thamani ya pesa kwa kidindi hicho. Hivo hizo micro finance institutions itawalazimu kuanza kutoa huduma kwa wateja wao ili waweze kuzalisha pesa nyingi zaidi zitakazowawezesha wao kulipa deni walilolipata toka katika mabenki ya kibiashara.
pesa za msaada(grants); hizi pesa zinakuwa zimetengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa kipindi husika. hivo hizi micro finance institutions itawalazimu kuomba hizo pesa kwa kuandaa andiko la mradi(project proposal) au mpango wa biashara(business plan) utakaoainisha mchanganuo mzima wa matumizi na mapato.
michango ya wanachama(venture capital); huu ni mtaji ambao unaotaka na michango mbalimbali ya wanachama kupitia akiba zao wanazoweka katika hiyo micro finance institutions kabla hawajaanza kukopeshana. mfano mzuri wa huu mtaji ni saccos. kupitia hiyo michango ndo inawawezesha kuanza kutoa huduma za kibenki kwa watu wengine.
hivo hizo ni baadhi tu ya zile nyingi ambazo hutumiwa na taasisi nyingi za kifedha katika kupata mitaji yao itakayowawezesha kutoa huduma za kibenki kwa watu. Nadhani ni wakati sahihi pia wa wadau mbalimbali kuitazama hii fursa kwa jicho pana zaidi ili uweze kujikita katika kufanya ili uweze kujiingizia kipato chako menyewe kwa kuamua kujiajili.
Pia husisahau kushare kwa wengine ili waweze kujifunza mambo mengi zaidi.
Pia husisahau kushare kwa wengine ili waweze kujifunza mambo mengi zaidi.
Nakubal sana mkuu keep it up afisa lisso
JibuFutashukrani sana broh....napambana mzee
JibuFutambona ya kwako uitumii broh
JibuFutaNitaanza hivi punde kuna mamb flani ya usajili sikukamilisha. Tutazjngumza kwanza this week
JibuFutahaina shaka nyumbi hii bombi hiii
JibuFuta