Fursa ya kibiashara na kujiendeleza kwa taasisi zinazotoa huduma za kibenki nchini Tanzania(micro finance institutions)...
Baada ya benki kuu ya Tanzania(B.O.T) kutangaza kuwa itapunguza kiwango cha riba kwa mabenki ya kibiashara mpaka kufikia asilimia kumi na moja(11%) imetafsiliwa kuwa ni fursa kwa taasisi zote za fedha zinazotoa huduma za kibenki kujipambanua zaidi katika kutoa huduma zao kwa watu wa hali ya chini na wasio kuwa na sifa ya kupata huduma za kibenki katika mabenki ya kibiashara kwa kuboresha huduma zao hususani kwa kuweka masharti ambayo kila mmoja ataweza kuyamudu kwa nafasi yake kwa sababu kwa sasa taasisi hizo za kifedha zitowazo huduma za kibenki zitakuwa zinapata mitaji yake ya kujiendesha zenyewe kwa riba nafuu mno toka katika mabenki ya kibiashara kwa sababu watakuwa na uwezo wa kurejesha hizo pesa baada ya kuziingiza katika mzunguko na kuzalisha.
Hivo ni vizuri kwa taasisi zote za fedha zinazotoa huduma za kibenki kujisajili na kufuata sheria sambamba na utaratibu wa nchi yetu katika kuendesha shughuli zake ili ziweze kunufaika na kunufaisha wateja wao katika kujikwamua na changamoto mbalimbali za kimaisha sambamba na kuleta maendeleo mbalimbali katika jamii zetu na taifa kwa ujumla. kwahiyo mazingira mazuri ya ufanyaji kazi tayari yameshaandaliwa hasa kupitia hatua hiyo ya kupunguza kiwango cha riba kwa mabenki ya kibiashara.
husisahau kufollow tovuti yetu ili uwe wa kwanza kupata taarifa punde tu baada ya kuchapicha chapisho letu katika tovuti.
Maoni
Chapisha Maoni