Maana ya microfinance institutions(taasisi za fedha zinazotoa huduma za kibenki), imeandaliwa na Florian Lisso


 Micro finance institutions ni asasi ndogo ndogo zote za kifedha ambazo zimejikita hasa kutoa huduma za kibenki kwa watu wenye hali duni ya kimaisha ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili katika maisha yao. Miongoni mwa hizo huduma za kibenki zinazotolewa na hizo taasisi za fedha ni huduma za mikopo(loans), huduma ya kuweka akiba(savings), kuhamisha pesa toka sehemu moja kwenda nyingine(funds transfer) sambamba na kupata huduma za bima(insurance). Mfano wa Asasi ndogo ndogo za kifedha ni saccos, vicoba, finca, pride na nyingine nyingi. Huduma za hizi asasi ndogo ndogo za kifedha hutolewa kwa lengo la kuwafikia watu ambao hawana sifa na vigezo za kupata huduma katika mabenki ya kibiashara kulingana na uwepo wa kanuni na taratibu zinazoaminika kuwa ni ngumu kwa wateja.

Hizi asasi ndogo ndogo za kifedha zina umuhimu na msaada mkubwa kwa watu hasa wale wenye hali duni ya kimaisha. Dhumuni kuu la hizi asasi ndogo ndogo za kifedha ni kutoa huduma za kibenki kwa watu ambao hawajatimiza sifa na vigezo vya kupata huduma katika mabenki ya kibiashara. Hivo yafuatayo ni miongoni mwa madhumuni ya asasi ndogo ndogo za kifedha kutoa huduma za kibenki kwa watu ni;

kupunguza umaskini; umaskini unapungua kutokana na watu kupata mikopo mbalimbali uenda ya rasilimali fedha au rasilimali vitu ambazo zitatumika katika uzalishaji wa kipato na utatuzi wa changamoto za kijamii na kiuchumi. pia micro finance institutions zinatoa huduma mbalmbali za bima kama bima ya afya, bima ya majanga na nyingine nyingi ambazo zitakuwa msaada kwa mtu pindi apatapo matatizo mbalimbali. 

kuboresha maisha ya watu; hao watu ni wale wenye hali duni ya kimaisha kwa kuwapatia mikopo ya fedha na rasilimali vitu vitakavowasaidia katika kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ili waweze kuzalisha kipato kitakachowasaidia kutatua chanmgamoto zinazowakabili.

kulinda fursa ya kibiashara kwa wakati; fursa ya kibiashara inaweza kulindwa na hizi micro finance kwa wakati kupitia kutoa mikopo kwa watu ili waweze kujikita katika shughuli za uzalishaji ili wazalishe kipato. hivo kitendo cha mtu kupata mkopo kwa wakati na kwenda kufanya shughuli ya kuzalisha pesa kwa wakati kulingana na fursa iliyopo inachukuliwa kama kuilinda hiyo fursa ya kibiashara ambayo ingeweza kumuingizia mtu kipato ambacho kingemsaidia katika kutatua changamoto zake mbalimbali za kimaisha.

usisahau kutufollow na kusubscribe blog yote ili uwe wa kwanza kupata taarifa zetu punde tu tukizichapisha.


Maoni

  1. Hongera sana mkuu nashauri andika makala nyingj zaidi na ni vizuri pia ukaweka menu na button mbalimbali za burudani, habari n.k

    JibuFuta
  2. shukrani sana broh kwa ushauri wako nitaufanyia kazi kaka

    JibuFuta
  3. Je vigezo vya kujiunga na hiyo tasisi ni vipi? 0767678809

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii