
HUYU NDIO MZAZI WA VICOBA(VILLAGE COMMUNITY BANK) VICOBA NI NINI?? Vicoba(village community bank) ni benki za kijiji zilizoanzishwa na watu kuanzia 15 mpaka 30 kwa lengo la kuweka akiba na kukopeshana kwa riba nafuu ambayo watakuwa wamekubaliana wanachama wenyewe kwa mujibu wa katiba yao. lengo la kuanzisha hizi benki ni kusaidiana ili waweze kupambana na umaskini sambamba na changamoto mbalimbali za kimaisha hasa za kiuchumi na kijamii. vicoba uendeshwa kwa katiba maalumu kulingana na makubaliano ya wanachama na pia katiba hizo lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria na kanuni za wizara husika kuanzia ngazi ya kata mpaka wilaya. MZAZI WA VICOBA "UPATU" ndio mzazi wa VICOBA(village community bank). Upatu ni mchezo unaotumiwa na watu mbalimbali kuchangiana fedha kisha baada ya fulani hizo fedha anapewa mtu na kuanza kuchangiana tena kwa ajili ya kupewa mtu mwingine kwa maana hizo fedha zinazochangishwa utolewa kwa mzunguko ili kilaaliyechangia lazima apate. le...