Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2018
Picha
TADB KUWASHIKA MKONO WAHITIMU VYUO VIKUU. Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB)imeazimia kuwashika mkono wahitimu wa vyuo vikuu hususani waliosomea masomo yanayohusu kilimo na uvuvi kwa kuwapatia mikopo mbalimbali ili waweze kutekeleza kwa vitendo vile walivyojifunza machuoni. kwa kufanya hivyo wanaamini watachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana sambamba na kukuza uchumi wa viwanda kupitia hiyo miradi itakayofanywa na hao wahitimu kwa kupitia hiyo mikopo itakayotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo.  Hivyo, sisi blog ya "ngalibanews" tunaipongeza benki ya maendeleo ya kilimo kwa kuwapatia hiyo fursa vijana ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kuthubutu na kuchangamkia hiyo fursa. Pia tunawashauri hao wahitimu katika masomo ya kilimo na uvuvi kujiunga pamoja na kuunda kikundi chao ambacho watakisajili kwa mujibu wa sheria na muongozo wa idara ya maendeleo ya jamii ili iwe rahisi kwao kupata huo mkopo na kutekeleza miradi yao a...
Picha
 TENGERU MARKET SACCOS KAA LA MOTO LA MAENDELEO Vyama vya Ushirika bado vina nafasi muhimu katika kuwaunganisha na kuwawezesha wananchi kubadili maisha yao na kujiendeleza kiuchumi.Aidha, Vyama vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) ni nyenzo ya kuwapatia wananchi mitaji kutokana na michango yao na mikopo kutoka katika vyombo na taasisi za fedha. TENGERU MARKET SACCOS NI NANI? Hiki ni chama cha ushirika kilichoundwa kwa umoja wa wafanyabiashara wanaopatikana katika soko la Tengeru lililopo wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha. Lengo la chama hiki cha ushirika nikubadili maisha ya wafanyabiashara hao kwa kuwaendeleza kiuchumi kwa kuwapatia mikopo mbalimbali itokanayo na michango yao kwa ajili ya kukuza biashara zao. KWANINI NI KAA LA MOTO? Tengeru market saccos ni kaa la moto la maendeleo kwa wanachama wake kwa sababu wameshindwa kutimiza lengo walilolikusudia pindi kinaanzishwa hiki chama.kwa takribani miaka zaidi ya mitano saccos hii ya soko la Tengeru haitoi huduma...