
KILICHOPO NYUMA YA PESA ZA VIJANA NA WANAWAKE HALMASHAURI Kwenye kila halmashauri nchini Tanzania kuna pesa zimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake. Pesa hizo zimetengwa kwa ajili ya kuwapa vikundi vya kimaendeleo ambavyo vimeundwa na hao vijana pamoja na hao wanawake. Na ili kila kikundi kiweze kupata hizo pesa ni lazima kiwe na shughuli maalumu ya uzalishaji mali ambazo zinawaingiza kipato sambamba na hivyo vikundi kutambulika kisheria yaani visajiliwe katika ofisi zenye mamlaka husika ambazo zipo chini ya usimamizi wa afisa maendeleo. KWANINI VIJANA NA WANAWAKE? Kwa sababu haya makundi mawili ndio chachu ya maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla kwa kuwa vijana ni taifa la kesho hivyo hakuna budi kuwawezesha sasa ili kesho waweze kusimama wenyewe na ukimuwezesha mwanamke mmoja ni sawa umeiwezesha jamii nzima kwa kuwa wanawake wanaangaliwa kama chachu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla kulingana na walivyobarikiwa. ...